Kaunti ya Marsabit inatazamiwa kuandaa maonyesho yake ya kwanza kabisa ya biashara kuanzia wiki hi Alhamisi katika uwanja wa Marsabit.
Hafla hiyo ya siku tatu itafunguliwa rasmi na Gavana Mohamud Ali mnamo Alhamisi, Septemba 14 na kufungwa na naibu wake Solomon Gubo Jumamosi, Septemba 16.
Angalau waonyeshaji 100 wanatarajiwa kuonyesha ubunifu, teknolojia, bidhaa na huduma zao kwa umma.
Kaulimbiu ya maonyesho ya kibiashara mwaka huu ni Kufungua fursa na uwezekano wa uwekezaji katika Kaunti ya Marsabit kupitia uongezaji thamani wa chakula na usalama wa lishe.
Kulingana na afisa mkuu wa Biashara na ushirika katika kaunti ya Marsabit Mahad Mohamed Dida amesema kwamba ni hafla ambayo inafanyika kwa mara ya kwanza kaunti ya Marsabit na kuwataka wafanyibiashara wote kujitokeza.