IDARA YA ELIMU KATIKA KAUNTI YA MARSABIT YAWEKA MIKAKATI KABAMBE KUZUIA VISA VYA UCHOMAJI WA SHULE KUTOKEA HAPA JIMBONI.
September 12, 2024
Na Samuel Kosgei
Ni afueni kubwa kwa wakaazi Oltorot lokesheni ya Mt. Kulal baada ya Kampuni ya kuzalisha nishati kutokana na upepo wa Lake Turkana Wind Power kuikabidhi rasmi wakaazi wa eneo hilo chumba kipya cha akina mama kujifungulia.
Kulingana na muuguzi wa kituo cha matibabu cha Olturot Brenda Akoth alisema kuwa chumba hicho kitawafaa sana akina mama kwani siku za nyuma akina mama wamekuwa wakijifungulia nyumba kutokana na ukosefu wa chumba cha kuzalia na pia umbali wa kituo cha afya wakati wa dharura.
Chumba hicho kipya anasema kina uwezo wa kumudu akina mama 10 kwa wakati mmoja.
Wakaazi wa Oltorot, Arapal, ngororoi, Sivicon na viungo vyake watafaidi na chumba hicho cha kujifungulia.
Wakaazi wa Oltorot wamesifia kuanzishwa kwa chumba hicho wakisema kitaokoa sana maisha ya akina mama na watoto watakaozaliwa.
Meneja wa uhusiano mwema wa kijamii Job Lengoiyap amesema kuwa jumba hilo limegharimu takribani shilingi milioni 11.1 kuikarabati.
Hivyo aliitaka jamii za eneo hilo kutumia chumba hicho kipya katika masuala yote ya akina mama na wototo ambao kwa miaka mingi wamekuwa wakihangahika.