Local Bulletins

Abiria Watatu Wafariki Baada ya matatu Kukanyanga Bomu la Kutegwa Ardhini Kaunti ya Mandera.

PICHA: KWA HISANI

Na Samuel Kosgei

Polisi walisema kuwa matatu hiyo iliyokuwa na abiria 14 ilikuwa ikielekea eneo la Takaba kutoka mji wa Mandera wakati ilipokanyanga bomu hilo kati ya Wargadud na Elele.

Inatajwa kuwa magaidi walikuwa wakilenga abiria ambaye siye mzaliwa wa eneo hilo ambaye aliyekuwa ndani ya gari hilo lakini alinusurika kwa kukimbilia msituni uliokuwa karibu kabla ya kuokolewa baadaye na polisi.

Waliojeruhiwa walikimbizwa hospitalini wakiwa na majeraha mengi.

Tukio hilo lilitokea saa chache baada ya maafisa wawili wa polisi na injinia mmoja wa eneo hilo kuuawa Jumanne katika shambulio kama hilo katika eneo la Tarbi na kufanya idadi ya waliouawa kuwa sita ndani ya saa 24.

Maafisa wengine watano walijeruhiwa katika tukio la Juni 20, kulinga na ripoti ya polisi.

Subscribe to eNewsletter