Local Bulletins

Rais William Ruto Aendelea Kutetea Mswada wa Kifedha 2023

Rais William Ruto | Picha: Kwa hisani

Na Adano Sharamo

Rais William Ruto amesisitiza kwamba mswada wa kifedha wa mwaka huu unalenga kufanikisha mipango yenye manufaa kwa wakenya ukiwamo ujenzi wa makazi bora kwa gharama nafuu.

Akizungumza wakati wa mpango wa kusambaza chakula shuleni Ruto amesema inasikitisha kuwaona wabunge wanaoishi kwenye mitaa ya kifahari wakiupinga mswada huo.

Kwa upande wake mwakilishi wa kike wa kaunti ya Nairobi Esther Passaris anaendelea kutetea msimamo wake wa kuunga mkono mswada huo kinyume na muelekeo wa kinara wake Raila Odinga.

Subscribe to eNewsletter