Local Bulletins

Viongozi wa Tana River, Isiolo na Marsabit Waahidi Kushirikiana na Serikali Kuimarisha Usalama

PICHA: KWA HISANI

Na Samuel Kosgei

Viongozi wa kaunti tatu za Tana River, Isiolo na Marsabit (TIM) ambayo ni sehemu ya eneo pana la kaskazini mwa nchini FCDC wameahidi serikali kuwa wamejitolea kushirikiana na serikali kuimarisha usalama katika maeneo yao.

Viongozi hao wakiongozwa na gavana wa Marsabit Mohamud Ali walimtaka waziri wa usalama Kithure Kindiki kuzidi kuwekaza nguvu za serikali katika kulinda wananchi wanaokumbwa na ukosefu wa usalama kwa muda haswa katika ukanda huu wa FCDC.

Aidha viongozi hao wa kaunti hizo tatu wameendelea kumshukuru rais kwa kuzidi kufanya uteuzi wa serikali kwa kuwapa nafasi wakaazi wa kaunti hizi tatu. Wanasema kuwa walioteuliwa watafanya kila wawezalo kutimiza ndoto ya serikali yake.

Subscribe to eNewsletter