Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
Na Adano Sharamo
Waakilishi wadi na maspika wao wana kila sababu ya kutabasamu baada ya tume ya kuratibu mishahara ya wafanyikazi wa umma SRC kuidhinisha mapendekezo ya nyongeza ya mishahara.
Katika taarifa mwenyekiti wa SRC Lyn Mengich amesema mapendekezo hayo yataanza kutekelezwa katika mwaka wa kifedha 2023/24.
Katika mapendekezo hayo yatakayotekelezwa katika awamu mbili maspika wa mabunge ya kaunti sasa watalipwa sh562, 312 kutoka sh525, 525 mapendekezo yakayoanza kutekelezwa kuanzia Julai 1.
Hata hivyo mshahara huo utaanza kuongezwa hadi sh601, 674 katika mwaka wa kifedha 2024/25 awamu ya pili ya mapendekezo yatakapoanza kutekelezwa.
Naibu spika naye atalipwa sh 231, 722 kutoka sh216, 563 wanazolipwa kwa sasa.
Katika awamu wa pili ya utekelezaji wa mapendekezo manaibu spika watalipwa sh274, 943 katika mwaka wa kifedha 2024/25.
Aidha watalipwa marupurupu ya sh62,000.
Nao kiongozi wa wengi na wachache watapata mshahara wa sh191,000 kutoka sh144,000 na sh 204, 716 katika mwaka ujao wa kifedha.
Pia watalipwa marupurupu ya sh62,400 kila mwezi.
Kuhusu waakilishi wadi SRC imeongeza mshahara hadi sh154, 481 mshahara ambao unatarajiwa kuongezwa hadi sh164, 588 mwaka ujao wa kifedha.
Haya yanajiri baada ya baadhi ya waakilishi wadi wakiwemo wa kaunti ya Marsabit kusitisha shughuli bungeni wakilalamikia mshahara duni.