Idadi chache ya wanafunzi waripoti shuleni wiki ya kwanza ya muhula huu…
January 10, 2025
Na Silvio Nangori,
Kwa mara nyingine tena waziri wa Elimu Profesa George Magoha amesisitiza kwamba hakutakuwepo na wanasiasa watakaoruhusiwa kuendesha shughuli zozote shuleni wakati huu wa mitihani wa kitaifa.
Magoha amewahakikishia walimu na wanafunzi kwamba usalama umeimarishwa katika maeneo ya mitihani ili kuhakikisha kwamba shughuli zote zinazofanyika bila tashwishi yoyote.
Amewarai wananchi kuwapa nafasi wanafunzi kufanya mitihani yao kwa Amani bila kuvurugwa kwa vyovyote vile.
Amesema kwamba watakaopatikana katika usumbufu karibu na shule, wizi wa mitihani au shughuli zingine amabazo hazifai katika shule watakashtakiwa na kukumbana na mkono wa sheria.