Wakaazi wa Karare, wanufaika na msaada wa chakula na vifaa vingine vya matumizi kutoka kwa katibu Kello Harsama.
January 9, 2025
Na Samwel Kosgei,
Mtu mmoja ameuawa kufuatia shambulizi la watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa Al Shabaab katika eneo la Bobo-Hindi kaunti ya Lamu.
Kulingana na ripoti za polisi, watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo walimteketeza John Moji hadi kutotambulika na baadaye kubomoa nyumba yake usiku wa kuamkia leo.
Akithibitisha kisa hicho, mwenyekiti wa Tume ya Kitaifa ya Huduma ya Polisi, Eliud Kinuthia amesema Moji alifariki akiwa amefungwa mikono nyuma ya mgongo wake, tukio sawa na watu wengine 6 waliouawa Jumatatu asubuhi.
Kinuthia anaamini kuwa washukiwa waliomvamia moji ndio wanaohusika na matukio ya mauaji.
Aidha amewapongeza polisi kwa hatua yao ya haraka ya kulilinda eneo hilo kabla ya washukiwa hao kuendeleza mauaji Zaidi.