Local Bulletins

Mandugu wawili wamuua baba yao kwa kumkataka kwa kisu katika eneo la Kiamisiori Bogetunya kaunti ya Kisii.

Picha: Hisani

Na Waihenya Isaac,

Polisi kaunti ya Kisii wanawasaka mandugu waliomuua baba yao kwa kumkataka kwa kisu katika eneo la Kiamisiori Bogetunya.

Kwa mujibu wa ripoti za DCI ni kuwa ndugu hao wawili Boniface Osoro na Getaro Osoro walimvamia baba yao mwenye umri wa miaka 60 baada ya majibizano madogo huku sababu mwafaka iliyopelekea unyama huo ikiwa bada haijajulikana.

Washukiwa hao ambao wamo mafichoni,wanaripotiwa kutoroka kisiri kabla ya wanakijiji wenye ghadhabu waliofika kumsaidia mzee baada yake kupiga kamsa kutaka kuwaadhibu.

Tayari polisi wamezidisha msako mkali dhidi ya ndugu hao wawili,huku uchunguzi ukiendelea ili kubaini chanzo cha mauaji hayo.

Subscribe to eNewsletter