WAUGUZI KATIKA KAUNTI YA MARSABIT WAMEAPA KUENDELEA NA MGOMO WAO HADI PALE SERIKALI YA KAUNTI YA MARSABIT ITAKAPOSHUGHULIKIA MATAKWA YAO YOTE.
September 19, 2024
Na Isaac Waihenya
Shughuli za watahiniwa kufanya mtihani wa darasa la nane KCPE zimesambaratika leo mchana katika eneo la Kapkusum,Muchongoi kaunti ya Baringo baada ya majambazi waliojihami kwa bunduki kuingia katika eneo hilo.
Watahiniwa wa KCPE katika shule za msingi za Kapchekir na Karne huko Baringo walitoroka shuleni pamoja na waalimu wao na wasimamizi wa mitihani wakati majambazi walianza kufyiatua risasi kiholela.
Wakti uo huo nyumba kadhaa zilichomwa katika uvamizi huo uliotekelezwa mchana kila mmoja akikimbilia usalama wake.
Mbali na nyumba, pia pikipiki moja iliyoachwa njiani na mmoja wa waliokuwa wanatoroka mashambulizi ya risasi kijijini pia ilichomwa.
Kulingana na wazee wa nyumba kumi ni kuwa mashambulizi hayo yamezua tararuki katika eneo hilo huku mipango ya kuona jinsi watahiniwa wa KCPE waliotoroka watakusanywa tena ili waendelee na mtihani wao.