Supkem Marsabit yaunga mkono wito wa kuwajibisha serikali ya Kenya Kwanza.
December 5, 2024
Na Samwel Kosgei,
Mke wa kiongozi wa ODM Raila Odinga, Ida Odinga, ameomba msamaha kuhusu matamshi aliyotoa kuhusu hitaji la kudhibiti makanisa ya nchini Kenya.
Ida alikuwa akizungumza mjini Kisumu Jumamosi wakati wa hafla ya Baraza la Kitaifa la Makanisa nchini (NCCK) ambapo alisema makanisa yaliyo chini ya baraza hilo yadhibitiwe ili kukuza uthabiti na umuhimu katika ujumbe wa kukuza uinjilisti nchini Kenya.
Sasa ameondoa matamshi yake, akisema kwamba alikuja kugundua kuwa maoni yake hayakuwa sawa na wengine.
Amesisitiza zaidi kwamba yeye ni mwamini aliyejitolea katika Yesu Kristo na ataendelea kujitolea kukuza ukuaji wa kanisa kwa jamii bora za humu nchini.