Idadi chache ya wanafunzi waripoti shuleni wiki ya kwanza ya muhula huu…
January 10, 2025
Na Denson Machuki,
Tume ya maadili na kupambana na ufisadi EACC imesema iko tayari kuwashtaki magavana watatu na madai ya ufisadi pindi tu afisi ya mkurugenzi wa mashtaka ya umma itakapoidhinisha mashtaka dhidi yao.
Afisa mkuu mtendaji wa tume hiyo Twalib Mbarak amesema kesi dhidi ya gavana wa Kirinyaga Anne Waiguru, Fahim Twaha wa Lamu na Dhadho Ghodana wa Tana River zimekuwa zikisubiri kwa muda ila pia si kwa sababu za kisiasa.
Mbaraka anasema wamechunguza vizuri na wana ushahidi wa kutosha dhidi ya magavana hao iwapo mkurugenzi wa mashtaka nchini Noordin Haji ataidhinisha.
Waiguru wa Kirinyaga anadaiwa kupokea shilingi milioni 10.6 za safari za kikazi alizozifanya au hata hazikufanyika. Swala hili lilitishia yeye kutimuliwa nje baada ya bunge la kaunti yake kumbandua japo akarejeshwa na bunge la seneti mwaka 2020.
Gavana wa Lamu Twaha anakumbwa na madai ya kuwaajiri watu kwa njia ya mapendeleo n ahata wengine wasiofuzu katika nyadhifa Fulani.
Gavana wa Tana River Ghodana anatakwa na EACC kwa madai ya ununuzi usiofuata sheria ambapo kaunti hiyo ilinunua magari na pikipiki bila kufuata sheria.