Local Bulletins

Bodi ya Shule ya msingi ya Songa yalalamikia ukosefu wa walimu shuleni humo.

Picha:Hisani

Na Waihenya Isaac,

TSC bado haijatimiza ahadi yake ya kuipa shule ya msingi ya Songa iliyoko lokesheni ya Karare kaunti hii ya Marsabit walimu watatu zaidi.

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa bodi ya shule hiyo Daniel Esimba Sele ni kwamba hadi kufikia sasa ni mwalimu mmoja pekee ambaye amefika shuleni humo kati ya watatu waliohadiwa na TSC.

Mwenyekiti huyo ametaja kuwa kwa sasa bado wanafunzi wanazidi kuadhirika kutokana na idadi ndogo ya walimu kwani kwani shule hiyo ina walimu sita pekee wanaofaa  kuwashughulikia takriban wanafunzi 400.

Aidha wametaja kuwa huenda wakaandaa maadamano iwapo tume ya TSC haitasuluhisha kero hilo haraka iwezekanavyo.

Kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa tume ya kuwaajiri wa walimu tawi la Marsabit TSC Russel Wafula ametaja kuwa tume hiyo iliwatuma walimu wote watatu shuleni humo huku akiahidi kufuatilia sababu ya wao kutoripoti kazini mwao hadi kufikia sasa.

Subscribe to eNewsletter