WAUGUZI KATIKA KAUNTI YA MARSABIT WAMEAPA KUENDELEA NA MGOMO WAO HADI PALE SERIKALI YA KAUNTI YA MARSABIT ITAKAPOSHUGHULIKIA MATAKWA YAO YOTE.
September 19, 2024
By Adano Sharawe,
Wizara ya Afya imeomba Shilingi bilioni 1.4 kutoka Wizara ya Fedha kupanua vituo vya kuhifadhi chanjo kote nchini na kununua vifurushi ambavyo vinaweza kuhifadhi chanjo hizo katika kiwango cha nyuzi kinachokubalika.
Mkuu wa jopo la kusambaza chanjo za kukabiliana na maradhi ya Corona Willis Akhwale, amesema vituo vinavyopatikana vinaweza kuhifadhi chanjo hizo kwa kiwango cha nyuzi kinachokubalika na pia kuhifadhi hadi chanjo milioni 20.
Akihutubia mkutano ulioandaliwa kwa njia ya mtandao na Chama cha Madaktari nchini, Dkt Akhwale amesema vifaa vyenye uwezo wa kudumisha kiwango cha joto kinachokubalika vinapatikana katika Taasisi ya Utafiti wa Matibabu Nchini (KEMRI) na vituo vingine vichache.
Ameongeza kuwa wizara inachukua tahadhari za kutochafua chanjo hizo.
Akhwale amesema ingawa Kenya imeagiza chanjo aina ya AstraZeneca-Oxford, bado inaweza kununua chanjo ya Pfizer, mara tu itakapopatikana na nafasi ya kuihifadhi kuwepo.
Akhwale alisema mpango huo utagharimu shilingi bilioni 34, ili kuchanja asilimia 30 ya idadi ya watu nchini kuanzia mwezi Machi mwaka huu hadi Juni 2023.