Local Bulletins

Waziri Magoha Awaonya Waalimu Wakuu Wanaowarudisha Nyumbani Wanafunzi Kwa Kukosa Kulipa Ada Ya Maendeleo Ya Shule

Waziri Wa Elimu Profesa George Magoha.
Picha;Hisani

By Adano Sharawe

Serikali Kupitia Wizara Ya Elimu Imewaonya Vikali Walimu Wakuu Wanaowarudisha Nyumbani Wanafunzi Kwa Kukosa Kulipa Ada Ya Maendeleo Ya Shule.

Akizungumza Alipozuru Shule Mbali Mbali Katika Kaunti Ya Nyeri Waziri Wa Elimu Prof George Magoha Ameonya Kuwa Mwalimu Yeyote Atakayemrudisha Mwanafunzi Nyumbani Kwa Kutolipa Ada Hio Ya Maendeleo Atachukuliwa Hatua Kali.

Amekiri Kwamba Janga La Corona Limeathiri Uchumi Wa Wazazi Kwa Hivyo Akawaomba Wakuu Washule Wasiwarudishe Nyumbani Watoto Kwa Sababu Ya Ada Ya Maendeleo Na Karo Bali Washauriane Na Wazazi Kuhusu Njia Za Ulipaji Wa Ada Hizo.

Wakati Uo Huo Ameweka Wazi Kuwa Serikali Itawasaidia Na Barakoa Wanafunzi Wanaosomea Katika Shule Zinazo Katika Maeneo Ya Mabanda Nchini Akisema Tayari Mikakati Imewekwa Kuhakikisha Wanafunzi Hao Wanapata Barakoa

Magoha Aidha Amesema Kuwa Walimu Wakuu Wanapaswa Kuzitumia Vyema Fedha Zilizotolewa Na Serikali Kusaidia Maendeleo Ya Shule Nchini.

Kulingana Na Magoha, Shilingi Bilioni Nne Zitaenda Kwa Shule Za Msingi Huku Shilingi Bilioni 14.6 Zikipelekwa Kwenye Shule Za Upili.

Aidha Waziri Magoha Anatarajiwa Pia  Kuangazia Idadi Kubwa Ya Wanafunzi Katika Eneo Hilo  Ambao  Wanatafuta Shule Mpya Baada Ya Shule Walizokuwemo Kufungwa.

 

Subscribe to eNewsletter