Local Bulletins

Wauguzi Wajiunga Na Matabibu Katika Kusitisha Mgomo Wao

Picha;Hisani

By Adano Sharawe,

Wauguzi wamejiunga na Matabibu katika kusitisha mgomo wao ambao umedumu kwa zaidi ya miezi mitatu kufuatia agizo la mahakama.

Katibu wa muungano wa wauguzi nchini KNUN Seth Panyako amewaagiza wauguzi kurudi kazini kufikia hapo kesho.

Jaji wa mahakama ya Leba Maureen Onyango mnamoJumatatu aliwaagiza wauguzi na matabibu kurudi kazini haraka iwezekanavyo huku akiagiza walipwe mishahara yao.

Wahudumu hao wa afya waligoma kulalamikia kutopandishwa vyeo, kupewa vifaa vya kujikinga wakiwa kazini, kucheleweshwa kwa mishahara miongoni mwa maswala mengine.

Subscribe to eNewsletter