Local Bulletins

Watu Tisa Wafariki Katika Ajali Iliyotokea Hii Leo Asubuhi Katika Eneo La Soysabu Gilgil Kwenye Barabara Kuu Ya Nakuru Kuelekea Nairobi.

 

Picha;Hisani

By Waihenya Isaac,

Watu tisa wamefariki katika ajali iliotokea hii leo asubuhi  katika eneo la Soysabu GilGil kwenye barabara kuu ya Nakuru kuelekea Nairobi.

Ajali hiyo iliyohusisha Matatu ya kampuni ya Mololine na Lori ilifanyika karibu na hospitali ya St Mary’s Ambapo tisa hao walifariki papo hapo.

Akidhibitisha Kisa hicho Kamanda wa polisi katika kaunti ndogo ya Gilgil,John Onditi amesema kuwa Matatu hiyo iligongana ana kwa  ana na lori hiyo ambayo ilikuwa ikilipita gari ndogo lililokuwa likielekea Nakuru kutoka Nairobi.

Onditi amesema kuwa watu wawili wamenusurika na wanapata matibabu katika hospitali ya St.Mary`s iliyoko Gilgil huku maiti za abiria waliofariki zikipelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha  hospitali ya kaunti ndogo ya Gilgil.

Aidha Oditi amewatahadharisha wahudumu wa matatu pamoja na abiria dhidi ya kukiuka sherea za trafiki akisema kuwa watakaokamatwa watachukuliwa hatua kali za kisheri.

 

Subscribe to eNewsletter