IDARA YA ELIMU KATIKA KAUNTI YA MARSABIT YAWEKA MIKAKATI KABAMBE KUZUIA VISA VYA UCHOMAJI WA SHULE KUTOKEA HAPA JIMBONI.
September 12, 2024
By Isaac Waihenya,
Wananchi wametakiwa kuwajibika wakti wa uchaguzi na kuwachagua viongozi wenye maadili.
Kwa mujibu wa kamishna wa tume ya Uiano na Utengamano Nchini NCIC Denvas Makori ni kuwa ni jambo la kusikitisha mno kuona kuwa wananchi wamekuwa wakiilaumu tume hiyo kutokana na ukosefu wa maadili kutoka kwa viongozi bila kuzingatia kuwa wao ndio waliowachagua.
Akizungumza na vyombo vya habari,Makori amesema kuwa tume hiyo inafanya kila jitihada kuhakikisha kuwa wanasiasa hawaenezi semi za chuki haswa wakti huu taifa linapoelekea katika uchaguzi mkuu mwaka ujao.
Kadhalika Makori amesifia hatua iliyopigwa na tume hiyo ya kuchapisha orodha ya Aibu huku akitaja kuwa imezaa matunda kwani wanasiasa wameaza kujizuia na semi za chuki na uchochezi ili kuzuia kuoorodheshwa katika orodha hiyo.