Local Bulletins

Walimu Walio Na Umri Wa Miaka 58 Na Zaidi Wafaa Tu Kurejea Kazini Kwa Hiari Yao – Nancy Macharia.

Katibu Mkuu Mtendaji Wa Tume Ya Huduma Za Walimu Nchini TSC Bi Nancy Macharia. Picha; Hisani

By Waihenya Isaac.

Wizara Ya Elimu Haitawalazimisha Walimu Walio Na Umri Wa Miaka 58 Na Zaidi Kusalia Nyumbani Iwapo Wanahitaji Kurejea Shuleni Kuendeleza Majukumu Yao Ya Kufunza.

Kwa Mujibu Wa Katibu Mkuu Mtendaji Wa Tume Ya Huduma Za Walimu Nchini TSC Bi Nancy Macharia Ni Kuwa Walimu Walio Na Umri Wa Miaka 58 Na Zaidi Wafaa Tu Kurejea Kazini Kwa Hiari Yao.

Mwaka Jana Serekali Iliwataka Wafanyikazi Waliozidi Umri Wa Miaka 58 Na Zaidi Kusalia Nyumbani Kama Njia Mojawepo Ya Kuwazuia  Dhidi Ya Hatari Ya Homa Ya Korona Iliyotajwa Kuwaadhiri Haraka Wakongwe, Watoto Pamoja Na Watu Wengine Wenye Matatizo Ya Kiafya.

Kauli Ya Bi Macharia Ilishabikiwa Na Waziri Wa Elimu Profesa George Magoha Ambaye Alitaja Kuwa Serekali  Itahakikisha Kuwa Shughuli Za Elimu Zitaendelea Bila Kutatizika Hata Licha Ya Walimu Hao Kukosekana Shuleni.

Aidha Waziri Magoha Ametetea Hatua Ya Wizara Hiyo Kuwazuia Wanahabari Kupata Habari  Shuleni Akisema Kuwa Serekali Imepiga Marufuku Watu Kutembelea Watoto Shuleni Kama Njia Mojawepo Ya Kuzuia Maambuki Ya Korona Kwa Wanafunzi.

Subscribe to eNewsletter