Local Bulletins

Wakazi Wa Kaunti Ya Samburu Waamrishwa Kuwasilisha Bunduki Haramu Ambazo Wanamiliki Kama Njia Moja Ya Kuimarisha Usalama Katika Kaunti Hiyo.

Picha;Hisani

By Waihenya Isaac,

Wakazi wa kaunti ya Samburu waamrishwa kuwasilisha bunduki haramu ambazo wanamiliki kama njia moja ya kuimarisha usalama Katika kaunti hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa polisi Katika kaunti ya samburi Samson Ogelo amesema kuwa Bunduki haramu kumi na saba zimetolewa mikononi mwa raia katika kipindi cha miezi miwili kufuatia ushirikiano wa serekali na wazee wa jamii.

Aidha Ogelo awaonya kuwa watakaokaidi amri ya kurejesha bunduki haramu watachukuliwa hatua kali za sheria

Vilevile amesisitiza kuwa oparesheni  ya kutwa Bunduki mikononi mwa raia itaendelea.

Subscribe to eNewsletter