Local Bulletins

Waiguru akosoa vikali hatua ya kutawazwa kwa spika Justin Muturi kuwa msemaji wa jamii za eneo la Mlima Kenya.

Gavana wa kaunti ya Kirinyaga Anne Waiguru.
Picha:Hisani

Na Adano Sharawe,

Gavana wa kaunti ya Kirinyaga, Anne Waiguru amekosoa vikali hatua ya kumtawaza spika wa bunge la Kitaifa Justin Muturi kuwa msemaji wa jamii za eneo la Mlima Kenya.

Kupitia ujumbe aliochapisha kwenye ukurasa wake wa Facebook na Twitter, gavana huyo amesema kuwa hafla kama ile haina maana kubwa sana kwenye siasa za eneo hilo.

Waiguru amesema kuwa hafla ile haitampa Muturi uongozi wa Mt Kenya kwani hiyo ni tamaduni iliyoletwa na wakoloni.

Ameongeza kuwa rais Kenyatta ambaye ndiye kiongozi wa Mt Kenya bado hajakiacha kiti chake na kitamaduni watu huwa hawarithi kiti wakati kiongozi bado yu hai.

Wakati yakijiri hayo, baadhi ya wazee kutoka jamii ya Agikuyu nao wamejitokeza kupinga kutawazwa kwa muturi huku wakidai kwamba inafanyika kisiasa na kwamba inaenda tofauti na tamaduni zao.

Hafla ya kumtawaza kwa Muturi inatarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi katika hekalu ya kitamaduni huko Kiambu.

Subscribe to eNewsletter