Marehemu padre Frank atajwa kama mtu mkarimu aliyependa kusaidia wasiojiweza katika jamii.
January 22, 2025
By Samuel Kosgei,
Wabunge wanaoegemea mrengo wa naibu wa rais William Ruto wameendelea kuukosa namna serikali inavyowabagua wabunge hao kwa kutowapa ulinzi kwenye mikutano yao na hata wakiwa kwenye shughuli zao za kawaida.
Wakizungumza katika makao ya naibu wa rais mtaani Karen wabunge hao Zaidi za 130 wamedai kuwa kulikuwepo na idadi ndogo ya polisi katika ukanda wa pwani hapo juzi kwenye mkutano wa naibu wa rais kinyume na viongozi wengine wanaounga mkono mchakato wa BBI na salamu za handsheki.
Akisoma taarifa hiyo kwa niaba kundi hilo mbunge wa Kilifi kaskazini Owen Baya amesema kuwa idara ya polisi imejiingiza katika hali ya kupendelea upande mmoja inapotoa ulinzi kwa viongozi suala analosema kuwa inspekta Hillary mutyambai anaafaa kuliangazia.
Aiadha wametoa wito kwa idara ya polisi na mahakama kutokubali kutumika na serikali kuvuruga au kudhulumu baadhi ya viongozi.
Vile vile wamenasema kuwa suala la BBI kwa sasa siyo muhimu kwa ikilinganishwa na matatizo wanayopitia wakenya huku akisoa namna wakenya wanavyolazimishwa kupitisha Bbi ikiwemo wawakilishi wadi. Badala yake wanasema kuwa ingekuwa bora iwwapo masuala ya referenda yatakuwa Zaidi ya moja iwapo ni lazima yafanyike.
Kwa upande wake mbunge wa Garissa Mjini Adan Duale amemshambulia kinara wa odm raila odinga kuhusiana na suala hilo la bbi akisema kuwa nyingi za kaunti zilizo katika maeneo kama zitapoteza mgao wa pesa kinyume na Raila alivyodai kuwa kaunti ya Turkana itaongezewa mgao iwapo BBI itapita.
Wakti uo huo wamesema kuwa upande wao upo tayari kukabiliana na wabunge wanaopanga kuwasilisha mswada wa kumbadua naibu wa rais bungeni siku ya bunge litakaporejelea vikao vyake.