Marehemu padre Frank atajwa kama mtu mkarimu aliyependa kusaidia wasiojiweza katika jamii.
January 22, 2025
By Samuel Kosgei,
Waakilishi wadi kaunti ya Isiolo waliounga mkono ripoti ya BBI wametaja ongezeko la mgao wa kaunti kutoka asilimia 15 hadi asilimia 35 na kutambuliwa kwa jamii ya wafugaji kama sababu kuu za wao kupitisha mswada wa BBI hapo jana
Waakilishi wadi hao wameunga mkono mswada huo licha ya kuwa kaunti ya isiolo itapoteza shilingi bilioni 1.3 kutokana na mfumo utakaotumika kugawa raslimali.
Waakilishi wadi ambao walipinga mswada huo wa BBI walisema kuwa hawakuridhishwa na habari kuwa kaunti hiyo itapoteza shilingi bilioni moja iwapo BBI itapitishwa na wakenya kwenye kura ya maoni
Wawakilishi wadi wanne ndio waliopinga ripoti hiyo ambao ni pamoja na; Abdi Sora Wa Garbartulla, Hassan Idd Bulapesa, Mohamed Jirmo Cherab na Isaack Abduba Fayo wa Kinna.
Tofauti na kaunti nyingine nchini ambapo shughuli ya kupitisha bbi imekuwa ikiongozwa na gavana wa kaunti, gavana wa kaunti ya isiolo mohammed abdi kuti hakufika katika kikao cha kujadili ripoti hiyo ya BBI