Marehemu padre Frank atajwa kama mtu mkarimu aliyependa kusaidia wasiojiweza katika jamii.
January 22, 2025
By Adano Sharawe,
Uongozi wa Chama cha Jubilee katika Bunge la Kaunti ya Nairobi umejitenga na matamshi ya Gavana wa zamani wa Nairobi Mike Sonko kuhusu ghasia za uchaguzi mkuu wa mwaka 2017.
Wakiongozwa na kiongozi wa wengi wa Bunge hilo Abdi Guyo, wameshutumu matamshi ya Sonko na kumtaka kubeba msalaba wake mwenyewe kwa kuzua ghasia hizo.
Guyo, ambaye pia ni MCA wa wadi ya Matopeni, amemdhubutu Sonko kuweka hadharani majina ya wale anaodai walihusika katika njama hiyo, huku akimuonya dhidi ya kukihusisha Chama cha Jubilee na siasa za deep state na system.
Guyo ametoa wito kwa Idara ya Upelelezi (DCI) kulichunguza swala hilo kwa haraka kwani ni lenye umuhimu kwa wakazi wa Nairobi na taifa zima.
Sonko alidai kwamba yeye pamoja na baadhi ya maafisa wa ngazi za juu serikalini walipanga njama ya kuzua ghasia baada ya uchaguzi huo ili kukifanya chama cha ODM kuonekana kibaya mbele ya Wakenya.