Padre Francisco (Frank) Terragni kupumzishwa hiyo kesho Alhamisi….
January 22, 2025
By Waihenya Isaac,
Tume Ya Uiano Na Utengamano Nchini NCIC Imewaonya Wanasiasa dhidi Ya Kutumia matamshi ya walala hoi na walala hai kwenye kampenzi zao kwa sababu yanalenga kuwagawanya wakenya.
Kwenye Kongamano la kuwahamasisha wanahabari Makamishna wa tume hiyo Philip Okundi Na Dorcas Kidogo wamesema kuwa matamshi hayo yatawagawanya wakenya na kuleta uhasama wakti taifa linapokaribia uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2022.
Aidha wamewarai wanahabari Nchini kuepuka machapisho potovu yanayoweza kuzua uchochezi humu Nchini.
Matamshi hayo yamekuwa yakitumiwa na baadhi ya viongozi Nchini ikiwemo Naibu wa Rais William Ruto.