Hali ya jua na ukavu kuzidi kushudiwa Marsabit na sehemu nyingi za nchi
January 7, 2025
By Samuel Kosgei,
Naibu katibu mkuu mpya wa chama cha Jubilee Joshua Kutuny amesema kuwa hawezi akachelea kuanzisha mswada wa kumtimua naibu wa rais William Ruto kutoka chama hicho tawala cha jubilee.
Hata hivyo Kutuny ambaye ni mbunge wa Cherangany amesema licha ya kuwa hajapokea taarifa zozote za kutimuliwa kwa naibu wa rais ataunga mkono mswada huo wa kutimuliwa kwake kwa ajili ya kumkosea nidhamu rais.
Kutuny ameteuliwa juzi kuwa naibu katibu wa jubilee akichukuwa nafasi yake Caleb Kositany ambaye ni mwandani wa naibu wa rais William Ruto. Hatua hiyo ilionekana kama kumkata mikono naibu wa rais ambaye anatajwa kama anayemkaidi rais.
Kutuny amekuwa mkosoaji mkuu wa naibu wa rais William Ruto ila alibadilisha mkondo huo 2013 alipoteuliwa kuwa mshauri wa kisiasa wa rais Uhuru Kenyatta.
Wiki jana naibu mwenyekiti wa Jubilee David Murathe alikuwa ameonya kutimuliwa kwa mbunge Kositany huku pia akidai naibu wa rais atafuata hivi karibuni.