Local Bulletins

Shirika la Human Rights Watch lasema Mahitaji ya Chanjo Yanakiuka Haki za Kenya.

Mmoja wa Wakenya akipokea chanjo ya Korona
Picha;Hisani

Na Samuel Kosgei,

SHIRIKA la haki za kibinadamu la Human Rights Watch imeedelea kushutumu hatua ya serikali ya Kenya kulazimishia wakenya kupokezwa chanjo ili kupokea huduma za kiserikali.

Masharti hayo ya kuzuia wakenya kupokea huduma za kiserikali yataanza kutekelezwa tarehe 21 Desemba 2021.

Kufikia mwishoni mwa mwezi Disemba takriban asilimia 10 ya watu wazima nchini Kenya ilikuwa wamechanjwa chanjo ya covid 19 kulingana na takwimu za Wizara ya Afya.

Kulingana na Adi Radhakrishnan, mtafiti mkuu katika shirika hilo amesema kuwa Kenya ipo katika hatari ya kukiuka haki za wakenya kwenye masuala ya kazi, afya, elimu, na usalama wa kijamii.

Mnamo Novemba 21 waziri wa afya, Mutahi Kagwe, alitangaza kwamba kuanzia Desemba 21, ofisi za serikali itahitaji mtu yeyote anayetafuta huduma za serikali kutoa uthibitisho wa chanjo kamili ya Covid-19.

Huduma zitakazoathiriwa ni pamoja na usafiri wa umma, elimu, uhamiaji, hospitali, na kutembelea magereza. Uthibitisho wa chanjo pia utakuwa wa lazima kwa kuingia katika mbuga za kitaifa, hoteli, na mikahawa.

Kulingana nao ni kuwa Kenya haina usambazaji wa kutosha wa chanjo za Covid-19 ili kuhakikisha kuwa watu wazima wote wanaweza kupata chanjo kwa muda uliowekwa na Wizara ya Afya.

Utoaji wa chanjo nchini ilianza ilianza mwezi Machi kipaumbele ikipewa wafanyikazi wa afya, walimu, maafisa wa usalama, na watu walio na umri wa zaidi ya miaka 58.

Kwa sasa, chanjo za AstraZeneca, Moderna, Pfizer, Johnson & Johnson, na Sinopharm zinapatikana nchini Kenya. Hata hivyo, takwimu za Wizara ya Afya zinaonyesha kuwa kuna utoaji mdogo sana wa chanjo nchini.

Kenya, ina wastani ya watu wazima milioni 27.2 na jumla ya watu milioni 55. Kufikia leo taifa limenunua au kupewa takriban dozi milioni 23 tangu kuanza kwa mpango wa chanjo.

Subscribe to eNewsletter