Idara ya Watoto Marsabit yawarai wazazi kuwarejesha wanao shuleni,muhula wa kwanza wa 2025….
January 8, 2025
By Waihenya Isaac,
Shirika la kutetea haki za binadamu la Haki Afrika limetishia kuwashtaki maafisa wa polisi wanaowaachilia huru washukiwa wa dhulma za kijinisia.
Afisa wa shirika hilo Abdulrahman Mwangoka amewataka wakuu wa idara ya polisi kufuatilia suala hilo ili maafisa hao wakabiliwe kisheria.
Mwangoka ameshtumu vikali hulka ya maafisa wa polisi ya kuwaachilia huru washukiwa wanaotekeleza visa vya dhulma katika jamii.
Aidha ameahidi kushirikiana na shirika hilo ili kuzuia ongezeko la visa hivyo.
Amesisitiza hoja ya polisi kuwakamata na kuwachukulia hatua za kisheria washukiwa wa dhulma hizo.