Local Bulletins

Serikali yaanza kuwahesabu wanyamapori katika kaunti ya Wajir.

Picha;Hisani

Na Radio Jangwani,

Serikali imeanzisha shughuli ya kuhesabu wanyamapori wanaoishi katika kaunti Ya Wajir kama njia moja ya kuimarisha mali asili katika maeneo hayo.
Hata hivyo kaunti hiyo ambayo hujivunia kuwepo kwa Aina ya twiga ambaye hufahamika kama “Somali Giraffe” inakabiliwa na changamoto za uwindaji haramu na pia ukame, huku Mamia ya wanyama hao wakisemekana kufariki katika kipindi Cha mwaka moja uliopita.
Twiga huyo hupatikana kila kona ya kaunti hiyo.
Kuhesabiwa huko ni kufuatia agizo la rais Uhuru Kenyatta la kutadhmini idadi ya maliasili kote nchini, zoezi hilo likitarajiwa kuleta manufaa kwa maeneo ambayo sekta ya kitalii imekuwa ikidorora.
Joseph Gathua ni mmoja wa wanasayansi wanaochukua data ya idadi ya wanyamapori kaunti ya Wajir.
Mwenyekiti wa uhifadhi kaskazini mashariki sharmarke sheikh takriban twiga 2000 wanapatikana kaunti ya Wajir.
Hata hivyo, mamia ya twiga waliangamia mwaka jana kutokana na uwindaji haramu ambao umekithiri na hali ya ukame.
Mwaka jana wakazi walieneza uvumi kwamba nyama ya twiga ni tiba ya virusi vya corona hali iliyosababisha wanyama hao kuuwawa.
Afisa mkuu wa shirika la kuhifadhi wanyamapori nchini kituo cha Wajir Kirimi Mbaka amesema wametia mbaroni zaidi ya watu 10 baadhi yao wakihukumiwa kifungo cha miaka 7 gerezani.

Subscribe to eNewsletter