Local Bulletins

Serekali Ya Kauti Ya Samburu Yamulikwa Tena Kwa Ufujaji Wa Fedha

Mhasibu Mkuu wa serikali Nancy Gathungu.
Picha:Hisani

By Waihenya Isaac,

Serikali ya Kaunti ya Samburu huenda ilitumia shilingi milioni 147 kulipia bili za miradi gushi wakati wa kipindi cha matumizi ya pesa za serikali cha mwaka 2018 /2019.

Kwa muijibu wa ripoti mpya kutoka kwa Mhasibu Mkuu wa serikali Nancy Gathungu, kaunti hiyo inadaiwa kuwa ililipa fedha hizo kwa Wizara za Maji, Mazingira na Kawi.

Kulingana na ripoti hiyo iliyowasilishwa kwenye Bunge la Seneti, Kaunti ya Samburu ilitoa malipo ya shilingi milioni 127.8 kwa Wizara ya Maji na shilingi milioni 19.88 kwa Wizara ya Kawi.

Hata hivyo, bili hizo hazionekani popote kwenye taarifa za kifedha za kaunti hiyo huku stakabadhi husika zikikosa kutolewa na hivyo kuibua wasi wasi kwamba huenda fedha hizo zilitumika kwa miradi isiyokuwepo.

Aidha wasi wasi umekuwepo kwamba kaunti nyingi na pia taasisi za serikali zinatumia billi gushi kama njia za kufuja fedha za umma.

Subscribe to eNewsletter