Idara ya Watoto Marsabit yawarai wazazi kuwarejesha wanao shuleni,muhula wa kwanza wa 2025….
January 8, 2025
By Waihenya Isaac
Serekali ya kaunti ya Wajir imeanza kutoa chanjo ya ugojwa wa korona hii leo kwa wahudumu wa wafya Katika hospitali ya rufaa ya kaunti hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari wakti wa Uzinduzi wa zoezi hilo, Afisa mkuu wa afya Katika kaunti hiyo Adan Eno amesema kuwa wahudumu wa afya, maafisa wa usalama pamoja na waalimu ndio watakaopewa kipau mbele.
Aidha mkurungezi wa afya Daktari Dahir Snow amesema kuwa awamu ya kwanza ya kutoa chanjo itaendelea kwa kipindi cha miezi miwili na kisha awamu ya pili itawalenga wale wenye zaidi ya umri wa miaka 50 mbali na wanaougua saratani.
Kamanda wa polisi Katika kaunti hiyo Stephen Ngetich neye amawataka wananchi kupuuza uvumi unaoenelezwa kuhusiana na chanjo hiyo huku akitaja kuwa iko salama kwao.