Marehemu padre Frank atajwa kama mtu mkarimu aliyependa kusaidia wasiojiweza katika jamii.
January 22, 2025
By Silivio Nangori,
Rais Uhuru Kenyatta amewapongeza wakilishi wadi mbali mbali Nchini waliopitisha mswaada wa maridhiano BBI.
Akizungumza katika eneo la kayole jijini Nairobi katika Hafla ya Kufuangua Hospitali,Rais amesema kwamba serikali yake itaendelea kushughulikia maendeleo ya nchi.
Aidha Kenyatta amewataka viongozi kuungana kutatua matatizo kwa sauti moja kuliko kuleta vurugu na tofauti miongoni mwa wananchi.
Amewataka viongozi wasitumie vyeo vyao kuwakandamiza na kuchochea watu kwa ajili ya ukabila kwa kila mkenya ana haki ya kuishi katika nchi ya Kenya.
Kuuhusiana na kuungana kwake na kinara wa ODM Raila Odinga, Rais Kenyatta amedai kuwa kumeleta Amani Nchini.
Aidha amewataka wananchi wote kuunga Mkono mswaada wa maridhiano BBI akidai kwamba una manufaa chungu nzima kwa mkenya wa kawaida.