Idara ya Watoto Marsabit yawarai wazazi kuwarejesha wanao shuleni,muhula wa kwanza wa 2025….
January 8, 2025
By Waihenya Isaac,
Oparasheni ya kuhakikisha kuwa wanafunzi wote waliomaliza darasa la 8 wanajiunga na shule za upili imeingia siku yake ya tatu hii leo.
Operesheni hiyo iliyoanzishwa siku ya jumatatu na waziri wa elimu Profesa George Magoha analenga kuhakikisha asilimia mia ya wanafunzi wanaojiunga na shule za sekondari.
Hii leo waziri Magoha alizuru mitaa ya mabanda ya Kisumu na kutoa hakikisho kuwa serekali itamuwezesha kila mwanafunzi aliyefanya mtihani wa KCPE kujiunga na kidato cha kwanza.
Aidha magoha ameelezea kurithishwa kwake na kaunti za Nyeri na Nyamira ambazo zimesajili asilimia 100 ya wanafunzi waliojiunga na kidato cha kwanza, kaunti ya Kisumu ikiwa na aslimia 82 huku ukanda wa pwani ukiwa na asilimia 70.