Idara ya Watoto Marsabit yawarai wazazi kuwarejesha wanao shuleni,muhula wa kwanza wa 2025….
January 8, 2025
Na Wahenya Isaac,
Tume ya uiano na Utengamano nchini NCIC itaendelea kuwaweka wanasiasa wanaoeneza semi za chuki katika orodha ya Aibu marufu kama “List of Shame”.
Kwa mujibu wa mwenyekiti wa tume hiyo Samuel Kobia ni kuwa idadi kubwa ya wanasiasa hawapendi kuwekwa kwenye orodha hiyo kwani huenda ikatia doa azma zao, hilo likisaidia katika kukabiliana na swala la uchochezi.
Kwenye mahojiano na runinga moja humu nchi,Kobia ametaja NCIC inafanya kazi kwa karibu na bunge la kitaifa ili kuhakikisha kuwa kuna sheria mwafaka itakayowazuia wanasiasa walionakesi za uchochezi mahakamani kugombea nyadhifa za kisiasa.
Amewataka wanasiasa kuuza sera zao kwa njia ya uadilifu bila kuchochea jamii nchini.