Local Bulletins

Museveni Atangazwa Rais Mteule Uganda

Rais Mteule Yoweri Kaguta Museveni.
Picha; Hisani

Yoweri Museveni ametangazwa kuwa rais mteule Uganda baada ya kupata ushindi wa kura asilimia 58.64.

Tume ya Uchaguzi Uganda (EC) imemtangaza Yoweri Kaguta Museveni kuwa mshindi wa uchaguzi mkuu uliofanyika Alhamisi tarehe 14 Januari 2021.

Kwa mujibu wa EC Museveni amepata kura 5,851,037 sawa na asilimia 58.64 ya kura zote zilizopigwa.

Mpinzani mkuu wa Museveni, mwanamuziki Robert Kyagulanyi, maarufu Bobi Wine, ameshika nafasi ya pili kwa kupata kura 3,475,398 sawa na asilimia 34.83 ya kura zote.

Bobi Wine hata hivyo alitangaza kutokukubaliana na matokeo hapo jana wakati tume ya EC ilipokuwa ikiendelea kutangaza matokeo.

Idadi kamili ya watu waliopiga kura ni 9,978,093 ikiwa ni sawa na asilimia 57.22 tu ya idadi ya watu waliojiandikisha kwenye daftari la wapiga kura.

Hii inamaana kuwa zaidi ya asilimia 40 ya waliojiandikisha hawakujitokeza kupiga kura.

Rais Museveni, ambaye amekuwa madarakani kwa miaka 35 akiwa atakuwa anaingia kuongoza kwa muhula wa sita.

Subscribe to eNewsletter