Mtu mmoja afariki kutokana na ugonjwa wa Kalazaar Marsabit, sita wakipokea matibabu kulingana na serikali ya kaunti.
February 21, 2025
By Waihenya Isaac
Waziri wa leba Simon Chilugui amekashifu mswaada wa mifungo unaolenga kudhibiti ufugaji wa nyuki akisema kwamba utawakandamiza wanaofanya biashara hiyo.
Waziri Chulugui amesema kuwa ipo wakaazi wanaotegemea nyuki kwa mapato yao na kuahidi kuwa mswaada huo hautaidhinishwa.
Mwaada huo unapendekeza marufuku ya kufuga nyuki Katika ardhi ya kibinafsi na kupendekeza maeneo kunakofugwa nyuki kusajiliwa rasmi.
Tayari biashara ya ufugaji nyuki imeonekana kuimarika mwaka huu baada ya kuadhirika mwaka jana kutokana na uvamizi wa nzige wa Jangwani ambao wafugaji wengi walilalama kuwa wadudu hao waharibifu waliharibu mimea inayowapa nyuki lishe ili kuzalisha asali.