Local Bulletins

Mswaada Wa Marekebisho Ya Katiba BBI Kuwasilishwa Bungeni Hapo Kesho.

Picha;Hisani

By Waihenya Isaac,

Rasimu ya Mswaada wa marekebisho ya Katiba ya mwaka 2020 BBI utawasilishwa bungeni hapo kesho.

Spika wa bunge la kitaifa Justin Muturi aliagiza mswada huo uwasilishwe bungeni kwa Usomaji wake wa kwanza.

Karani wa Bunge ameelekezwa kupata nakala za kutosha za Mswaada huo.

Nakala hizo zinapaswa kuwa katika mfumo ambao Mswaada uliwasilishwa kwa mabunge ya kaunti 47 na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka IEBC kuwezesha kuingizwa katika bunge kama ilivyoelekezwa.

Kufikia sasa,kaunti 43 zimepitisha Mswaada wa BBI na tatu ambazo ni ElgeyoMarakwet,Nandina Baringo  wameukataa mswada huo.

Subscribe to eNewsletter