Local Bulletins

Michuano ya kuwania kombe la EURO 2020 awamu ya raundi ya 16 kuendelea wikendi hii.

Picha:Hisani

By Waihenya Isaac,

Michuano ya kuwania kombe la EURO mwaka wa 2020 inatarajiwa kuendelea hapo kesho baada ya mapumziko ya siku mbili.

Wales iliyomaliza ya pili katika kundi A nyuma ya Italia, itafungua awamu ya raundi ya 16 bora itakapokabiliana na Denmark iliyomaliza ya pili katika kundi B.

Mechi hiyo itasakatwa katika uga wa Johan Cruijff Arena nchini uholanzi kuanzia saa moja jioni.

Mshindi kati ya Wales dhidi ya Denmark atachuana na mshindi kati ya Uholanzi na Jamhuri ya Czech katika awamu ya robo fainali.

Katika mechi nyingine, bingwa wa taji hilo mwaka wa 1968, Italia atachuana na Austria waliomaliaza katika nafasi ya pili katika kundi C katika uga Wembley jijini London Uingereza.

Mshindi kati ya mechi hii atachuana na mshindi kati Ubelgiji na Ureno katika awamu ya robo fainali.

 

Subscribe to eNewsletter