Local Bulletins

Makundi mbalimbali yanazidi kujitokeza kuwatetea majaji waliotoa uamuzi unasimamisha mchakato wa kubadilisha katiba kupitia BBI.

Picha;Hisani

Na Waihenya Isaac

Makundi mbalimbali yanazidi kujitokeza kuwatetea majaji waliotoa uamuzi unasimamisha mchakato wa kubadilisha katiba kupitia BBI.

Muungano wa wanasheria wa kimataifa ICJ tawi la Kenya umekuwa wa hivi punde kuwasuta wanasiasa kwa kuendelea kuwashambulia majaji waliotoa uamuzi huo.

Kupitia kwa mwenyekiti wake Kelvin Mogeni, ICJ imesema inasimama na idara ya mahakama kwa misingi kwamba mchakato wa BBI unajaribu kutumia njia za mkato kubadilisha katiba kinyume na matakwa ya Wakenya.

Zaidi ya hayo, ICJ imemtaka mwanasheria mkuu Kihara Kariuki kujitokeza waziwazi na kukemea tabia hii ya baadhi ya viongozi na pia kujitenga na misimamo mikali dhidi ya maamuzi ya mahakama inayotolewa na viongozi.

Subscribe to eNewsletter