Serikali ya kaunti ya Marsabit yakana madai ya unyakuzi wa ardhi na kutenga jamii ya Sakuye katika harakati ya kufunguliwa kwa mgodi wa Dabel.
January 13, 2025
Na Waihenya Isaac
Mkugenzi katika idara ya hali ya anga kaunti ya Marsabit Roba Ali amesema kilimo kwenye kaunti ya Marsabit kimeadhirika kwa kiwango kikubwa kutokana na mabadiliko ya tabia nchi.
Kwa mujibu wa Roba ni kwamba hali hiyo imesababisha ukosefu wa mvua na kuchangia kwa wakulima kupata mazao duni.
Mabadiliko hayo ambayo ameyataja kusababishwa na uharibifu wa mazingira yamefanya mvua kuwa chache na kipindi cha kiangazi kuwa kirefu.
Hata hivyo Roba amewahimiza Wakulima kufuatilia habari za hali ya anga kila wanapojiandaa kwa shughuli za upanzi.
Ametaja kuwepo kwa ushirikiano kati yao na wananchi ili kuwazuia dhidi ya hasara.