Local Bulletins

Kiongozi Wa Chama Cha ODM Raila Odinga Amesema Chama Chake Kitalinda Vilivyo BBI Na Handisheki.

Kinara Wa ODM Raila Odinga Akiipigia Debe Ripoti Ya BBI.
Picha Hisani

By Adano Sharawe,

Kiongozi Wa Chama Cha ODM Raila Odinga Amesema Chama Chake Kitalinda Vilivyo BBI Na Handisheki.

Akizungumza Alipoongoza Mkutano Wa Magavana Wa Chama Hicho Hii Leo, Odinga Amewataka Viongozi Hao Kuwa Katika Mstari Wa Mbele Kuilinda Vilivyo Ripoti Hiyo Kutoka Kwa Watu Anaosema Wanalenga Kuwapotosha Wakenya Kuihusu.

Waziri Huyo Mkuu Wa Zamani Aidha Ametoa Hakikisho Kwamba Handisheki Baina Yake Na Rais Uhuru Kenyatta Imesalia Imara Licha Ya Madai Kuwa Chama Hicho Kinapanga Kujiondoa.

Miongoni Mwa Waliohudhuria Mkutano Huo Ni Manaibu Viongozi Wa Chama Hicho Hassan Joho Aliyepia Gavana Wa Mombasa Na Gavana Wa Kakamega Wycliffe Oparanya.

Subscribe to eNewsletter