Marehemu padre Frank atajwa kama mtu mkarimu aliyependa kusaidia wasiojiweza katika jamii.
January 22, 2025
By Samuel Kosgei,
Jamii ya wasomali ya Harti na Issack inaoishi katika kaunti hii ya Isiolo wameelezea dhulma ya kihistoria waliopitia mwaka 1965 iliowaacha umasikini.
Dhulma hizo ni zikiwemo kunyanyaswa na hata kupokonywa ardhi walizokuwa wanamiliki wakati huo.
Kulingana na jamii hiyo ni kuwa walipitia hali ngumu kwa kupoteza mali yao na kubaki masikini wasijue la kufanya.
Jamii hiyo imetaka serikali ya kaunti na serikali ya kitaifa kuzingatia maslahi yao ili wapate haki yao ya kisheria kwani wanadai kutengwa na serikali.
Hata hivyo wamesifia utawala wa aliyekuwa gavana wa kaunti ya Isiolo Godana Doyo wakisema kuwa alikuwa anazingatia maslahi yao tofauti na gavana wa sasa Mohamed Abdi Kuti.
Jamii hiyo imelalamikia kubaguliwa na serikali ya kaunti ya Isiolo kwa kushindwa kuajiri kazi vijana wao.