Local Bulletins

Kasisi Mmoja Katika Kaunti Ya Kirinyaga Akabiliwa Na Mashataka Ya Kuwanajisi Na Kuwapa Ujauzito Wanawe Wawili Wenye Umri Wa Miaka 14 And 16 Mtawalia.

Picha; Hisani

By Jilo Dida.

Kasisi Mmoja Katika Eneo  La Ndia Kaunti Ya Kirinyaga Anakabiliwa Na Mashataka Ya Kuwanajisi Na Kuwapa Ujauzito Wanawe Wawili Wenye Umri Wa Miaka 14 And 16 Mtawalia.

Mshukiwa  Huyo Kwa Jina  Guchina Mwenye Umri Wa Miaka 51 Atasalia  Rumande Hadi Siku Ya Alhamisi Januari 7 Baada Ya Kukiri Makosa Yake Mbele Ya Hakimu Mkaazi Antony Mwicigi Wa Mahakama Ya Baricho.

Kulingana Na Mashataka Ni Kuwa Mshukiwa Alitekeleza Tendo Hilo Kwa Mtoto Wa Kwanza Kati Ya Tarehe Mosi Na Tarehe 30 Mwezi Juni Mwaka Wa 2019 Na Kwa Mtoto Wa Pili Kati Ya  Tarehe Mosi Hadi 30 Mwezi Agosti 2020 Katika Kijiji Cha Kianyakiru Eneo Bunge La Ndia.

Kiongozi Wa Mashataka Patricia Gikunju Hata Hivyo Ameomba Mahakama Kupewa Hadi Tarehe 7 Kumaliza Uchunguzi Wake Ya Kusanya Stakabadhi Za Watoto Hao.

Mushukiwa Alikamatwa Na Maafisa Wa Polisi Baada Ya Uchunguzi Wa Kina Katika Eneo La Mbeere Kusini Alikokuwa Mafichoni Mapema Mwezi Jana.

Mtoto Wa Kwanza Ana Ujauzito Wa Miezi 7 Huku Wa Pili Akiwa Na Ujauzito Miezi 5.

Subscribe to eNewsletter