Marehemu padre Frank atajwa kama mtu mkarimu aliyependa kusaidia wasiojiweza katika jamii.
January 22, 2025
By Waihenya Isaac,
Kamati ya kitaifa ya mpango wa BBI imetaja kuwa itanza kampeni za kupigia debe Ripoti hiyo kuanzia jumatatu wiki ijayo.
Kwa mujibu wa viongozi wa kamati hiyo,Junet Mohamed na Denis Waweru ni kuwa mipango ya kuanza kampeni za kuipa umaarufu zaidi ripoti ya BBI imekamilika.
Viongozi hao walikuwa wameandaa kikao cha pamoja na wabunge tofauti walioyapongeza mabunge ya kaunti kwa kupitisha mswaada huo na kuuelekeza katika hatua nyingine.
Aidha wameitaka idara ya Mahakama kuharakisha kesi zilizowasiliswa mahakamani kupinga mswada huo ili isiadhiri mipango ya kura ya maoni.
Kadhalika Wabunge waliohudhuria kikao hicho wameahidi pia kuupisha mswaada huo bungeni.
Kufikia sasa mabunge 41 ya kaunti yamepitisha mswada huo, huku Bunge la Kaunti ya Baringo likiwa la kipekee lililoukataa.