Local Bulletins

Jamaa Za Waadhiriwa Wa Mkasa Wa Mauaji Ya Wagala Kaunti Wajir Bado Wanadai Haki Miaka 37 Baada Ya Unyama Huo Kufanyika.

Picha;Hisani

By Waihenya Isaac

Jamaa za waadhiriwa  wa mkasa wa  mauaji ya Wagala kaunti Wajir bado wanadai haki miaka 37 baada ya unyama huo kufanyika.

Wakizungumza jiji Nairobi Katika maadhimisho ya kukumbuka siku ilipotokea mauaji hayo,Jamii ya Degodia ameitaka serekali kuwalipa fidia waadhiriwa kama ilivyopendekezwa na Ripoti ya Kweli haki na maridhiano TJRC.

Wamtaka Rais Uhuru Kenyatta kuingilia kati ili kuharakisha zoezi la kuwafidia waadhiriwa hao ambao wametaja kuwa limechukua kipindi kirefu kutekelezwa.

Mauaji hayo yalifanyika Katika uwanja mdogo wa  ndege wa Degodia Ambapo wanaume wa jamii ya Degodia walikusanywa na kuwekwa kwenye jua kali bila maji wala chakula kwa siku kadhaa.

Subscribe to eNewsletter