Jimbo katoliki la Marsabit laadhimisha miaka 60 ya kueneza Injili.
November 23, 2024
By Waihenya Isaac,
Bunge la kitaifa litampiga msasa jaji Martha Koome tarehe 13 mwezi Mei mwezi mwaka huu, baada ya Jaji Koome kupendekezwa na tume ya huduma za mahakama JSC kuwa jaji mkuu.
Koome anatarajiwa kufika mbele ya kamati ya mbunge Kuhusu sheria kwa Mahojiano.
Aidha Umaa umetakiwa kuwasilisha maoni yao kufikia tarehe 12 mwezi Mei mwaka huu kuhusiana na zoezi la mahojiano ya jaji huyo wa mahakama ya Rufaa.
Bunge litanganzia mahojiano na Ripoti ya kamati hiyo ya Bunge na iwapo litaridhia,Rais Kenyatta atamteua rasmi jaji Koome kuwa jaji mkuu kujaza nafasi iliyowachwa wazi na Jaji mkuu David Maraga aliyestafu tarehe 12 mwezi januari mwaka huu.
Koome ambaye amehudumu kwa kipindi cha miaka 33 alikuwa miongoni mwa watu kumi waliohojiwa na tume ya huduma za mahakama JSC wiki jana hii ikiwa mara yake ya pili kutafuta kiti hicho.