Local Bulletins

IMF Kukopesha Kenya Sh262b Kufufua Uchumi

Picha;Hisani

By Samuel Kosgei,

MAAFISA wa Shirika la Fedha Ulimwenguni (IMF) wanaozuru Kenya wametangaza kuwa shirika hilo litaipa Kenya mkopo wa Shilingi  bilioni 262.7

Katika taarifa kutoka ujumbe wa shirika hilo mkopo huo ambao utatolewa kwa kipindi cha miezi 38 ijayo utatumika kufadhili mipango ya kupambana na athari za Covid-19 kwa uchumi

Ujumbe huo umekuwa ukikutana na maafisa wa Kenya kwa njia ya mtandao kuanzia Desemba 9 hadi Desemba 17 mwaka jana. Hata hivyo, ulikamilisha utathmini wake mnamo hapo jana.

Wanachama wa ujumbe huo walifanya mikutano na Waziri wa Fedha Ukur Yatani, Gavana wa Benki Kuu Nchini (CBK) Patrick Njoroge, Mkuu wa Utumishi wa Umma Joseph Kinyua, miongoni mwa maafisa wengi wa ngazi ya juu katika serikali ya Kenya.

Subscribe to eNewsletter