Local Bulletins

IEBC Yawaonya Wanaopanga Kuwania Nyadhfa Mbalimbali Za Kisiasa Katika Uchaguzi Mkuu Mwaka Ujao Dhidi Ya Kutumia Stakabadhi Gushi Za Masomo.

 

Picha; Hisani.

By Radio Jangwani,

Watu wanaopanga kuwania nyadhfa mbalimbali za kisiasa katika uchaguzi mkuu mwaka ujao wameonywa vikali dhidi ya kutumia stakabadhi gushi za masomo.

Tume ya Uchaguzi IEBC imesema inashirikiana kwa karibu na Mamlaka ya Kitaifa ya Kuhitimu Kenya National Qualifications Authority  ili kutambua stakabadhi gushi zitakazowasilishwa na wawaniaji mbalimbali.

Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati amesema wanatarajia takribani wagombea zaidi ya elfu ishirini kwenye nyadhfa mbalimbali mwaka 2022.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mamlaka hiyo Kilemi Mwiria amesema amekutana na IEBC kupanga mikakati kuhusu jinsi watakavyoshughulikia suala hilo.

Mwiria amesema miongoni mwa mikakati hiyo ni kuhakikisha kwamba vyeti vyote vya masomo vitakavyowasilishwa vitatathiminiwa kabla ya yeyote kuidhinishwa.

Kulingana na sheria za uchaguzi wawaniaji wa nyadhfa za ugavana na urais wanahitajika kuwa na digrii. Aidha marekebisho yaliyofanyiwa sehemu ya 22 ya sheria za uchaguzi ni kwamba kuanzia mwaka 2022 yeyote atakeyewania wadhfa wa uwakilishi wadi, ubunge na useneta sharti awe na digrii.

Suala kuu lililochangia kuwekwa kwa masharti hayo ya masomo ni kuhakikisha viongozi wanaochaguliwa wanaelewa masuala muhimu, hasa wabunge na wawakilishi wadi ambao wanahusika katika kutunga sheria na kupitisha miswada mbalimbali.

Subscribe to eNewsletter