WAUGUZI KATIKA KAUNTI YA MARSABIT WAMEAPA KUENDELEA NA MGOMO WAO HADI PALE SERIKALI YA KAUNTI YA MARSABIT ITAKAPOSHUGHULIKIA MATAKWA YAO YOTE.
September 19, 2024
Picha;Hisani
By Jillo Dida.
Tume ya maadili na ufisadi nchini EACC imewahoji wawakilishi wadi 13 kutoka bunge la kaunti ya Baringo kufuatia kizaza kilichoshuhudiwa katika bunge hilo wiki iliyopita wakati wa mjadala wa mchakato wa kubadilisha katiba kupitia BBI.
Alhamisi iliyopoita bunge la kaunti ya Baringo ilikuwa bunge la kwanza kuangusha mchakato wa BBI hatua ambayo ilipelekea machafuko katika bunge hilo.
Tume ya EACC inataka kujua MCAs ambao walikiuka uongozi na maadili wakati wa kikao cha Bunge hilo na waliosababisha machafuko hayo.
Miongoni mwa watu waliohojiwa na kuandikisha taarifa kuhusiana na machafuko hayoo ni ikiwemo Spika wa bunge la Baringo David Kiplagat, Naibu wake Jacob Cheboiwo, karani wa bunge hilo Richard Koech, maafisa watatu wa ulizi pamoja na wawakilishi wadi 12.
Kamishona wa EACC ukanda wa kusini mwa bonde la ufa Hassan Khalid katika barua yake February 18 kwa karani wa bunge hilo, ameamuru wawakilishi wa wadi waliotajwa kufika katika ofisi za EACC Nakuru kuhojiwa na kurekodi taarifa kati ya tarehe 22-24 mwezi Februari.
EACC pia inataka karani wa bunge hilo kusalimisha rekodi ya kanda ya Hansard wakati wa kikao hicho.