WAUGUZI KATIKA KAUNTI YA MARSABIT WAMEAPA KUENDELEA NA MGOMO WAO HADI PALE SERIKALI YA KAUNTI YA MARSABIT ITAKAPOSHUGHULIKIA MATAKWA YAO YOTE.
September 19, 2024
By Grace Gumato
Na katika mahakama hiyo hiyo ya Marsabit, dereva aliyehusika katika ajali ya Hulahula iliyowaua watu wawili amewasilishwa mahakamani.
Isaya Roble Elsimonte alifikiwa mbele ya hakimu Tom Mbayaki na kushtakiwa kwa mashataka ya mauaji ya kukusudia kwa kuendesha gari vibaya kinyume na sheria.
Elsimote alikamatwa siku ya Jumatatu wiki hii ikiwa ni wiki mbili tangu gari aina ya probox alilokuwa akiendesha kuhusika katika ajali na kusababisha vifo kule Hula Hula viungani mwa mji wa Marsabi kwenye barabara kuu ya Marsabit-Isiolo, tarehe 8 mwezi huu.
Mshukiwa alifikishwa mbele ya hakimu Tom Mbayaki Wafula ambapo alikanusha mashtaka.
Hakimu Wafula alimuachilia kwa dhamana ya shilingi elfu ishirini kusubiri kusikizwa tena kwa kesi hiyo tarehe 12, Julai mwaka huu.